Posts

Showing posts from November, 2022

Mwanzo 2

MLANGO WA 2 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. 2  Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3  Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. 4  Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi 5  hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; 6  ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi. 7  Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. 8  Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya. 9  Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa ma...

Mwanzo 1

  MLANGO 1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2  Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3  Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4  Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. 5  Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. 6  Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. 7  Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. 8  Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili. 9  Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. 10  Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 11  Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na...